• HABARI MPYA

  Thursday, July 22, 2021

  REAL MADRID YAMTAMBULISHA RASMI BEKI MPYA DAVID ALABA


  BEKI wa kimataifa wa Austria, David Alaba anayeweza kucheza kama kiungo wa ulinzi pia, jana ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa Real Madrid baada ya kusaini mkataba Mei 28 kufuatia kumaliza mkataba Bayern Munich.
  Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano baada ya kuondoka Bayern alikocheza mechi 431 ndani ya miaka 13, akishinda mataji 10 ya Bundesliga na mawili ya Champions League.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YAMTAMBULISHA RASMI BEKI MPYA DAVID ALABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top