• HABARI MPYA

  Tuesday, July 20, 2021

  AZAM FC YASAJILI MCHEZAJI MPYA WA TATU KUELEKEA MSIMU UJAO, SAFARI HII NI NYOTA MZAWA EDWARD CHARLES MANYAMA KUTOKA RUVU SHOOTING


  KLABU ya Azam FC imemsajili beki wa kushoto wa kimataifa wa Tanzania, Edward Charles Manyama kutoka Ruvu Shooting ya Pwani kwa mkataba wa miaka mitatu utakaomfanya adumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2024.
  Manyama ni mmoja wa mabeki wa kushoto wanaoendelea kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, hivyo anatarajiwa kwenda kuendeleza makali yake ndani ya kikosi cha Azam FC.
  Huyo anakuwa mchezaji mpya wa tatu kusajiliwa Azam FC kuelekea msimu ujao, baada ya nyota wa kimataifa wa Zambia, kiungo mshambuliaji, Charles Zulu na mshambuliaji, Rodgers Kola.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YASAJILI MCHEZAJI MPYA WA TATU KUELEKEA MSIMU UJAO, SAFARI HII NI NYOTA MZAWA EDWARD CHARLES MANYAMA KUTOKA RUVU SHOOTING Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top