• HABARI MPYA

  Sunday, July 04, 2021

  MILWAUKEE BUCKS YATINGA FAINALI YA YA KWANZA TANGU 1974

   LICHA ya kumkosa MVP mara mbili, Giannis Antetokounmpo, Milwaukee Bucks imetinga Fainali ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani, maarufu kama NBA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974 baada ya kuichapa Atlanta Hawks 118-107 katika Game 6 ya fainali ya Eastern Conference Alfajiri ya leo.
  Ushindi huo umetokana na mchango mkubwa wa Khris Middleton aliyefunga pointi 32, zikiwemo pointi 16 mfululizo katika kota ya tatu iliyoamua mchezo.
  Kwa matokeo hayo, Milwaukee inatinga fainali kwa ushindi wa jumla wa series 4-2 na itakutana na Phoenix Suns, washindi wa West – Game 1 ya kwanza itakuwa Alfajiri ya Jumatano huko Phoenix.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MILWAUKEE BUCKS YATINGA FAINALI YA YA KWANZA TANGU 1974 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top