• HABARI MPYA

  Saturday, July 24, 2021

  KOCHA MFARANSA WA SIMBA SC, DIDIER GOMES ASEMA ANATAKA KUSHINDA KOMBE LA TFF KESHO AMALIZE MSIMU VIZURI

  KOCHA Mfaransa wa Simba SC, Didier Gomes Da Rosa amesema kwamba anataka kushinda Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kesho Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigom ili amalize msimu vizuri.
  Akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari leo mjini Kigoma kuelekea kwenye mchezo wa fainali dhidi ya watani wa jadi, Yanga SC, Gomes amesema baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ni muhimu wakachukua na Kombe la TFF pia. 
  “Tunataka kumaliza msimu huu vizuri, tunataka kuwafurahisha mashabiki wetu lakini pia ni muhimu sana kushinda kombe hili ili iwe mara ya pili. Kesho tutakuwa na mchezo wa aina nyingine na nawaamini wachezaji wangu wanataka kushinda,”amesema Gomes.


  Kwa upande wake, Nahodha Msaidizi wa Simba SC, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amesema kwamba anafurahi wamejiandaa vizuri na kilichobaki ni kwenda kufanya kazi.
  “Maandalizi yameenda vizuri na sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri. Tunajukumu kubwa sana kwa timu yetu na kufanya vizuri kesho ndio italeta taswira ya ukubwa wa Simba,” amesema Tshabalala. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA MFARANSA WA SIMBA SC, DIDIER GOMES ASEMA ANATAKA KUSHINDA KOMBE LA TFF KESHO AMALIZE MSIMU VIZURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top