• HABARI MPYA

  Monday, July 19, 2021

  AZAM FC YASAJILI MSHAMBULIAJI MZOEFU WA KIMATAIFA WA ZAMBIA, RODGERS KOLA KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI


  KLABU ya Azam FC imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Rodgers Kola, kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Zanaco ya kwao. 
  Mshambuliaji huyo mzoefu, mrefu na mwenye umbo kubwa, amesaini mkataba mbele ya Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', utakaomfanya kudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2023.
  Kola aliyefunga jumla ya mabao 14 katika mashindano mbalimbali nchini Zambia, anakuja Azam kuongeza nguvu kwenye safu yetu ya ushambuliaji, kuanzia msimu ujao 2021/2022.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YASAJILI MSHAMBULIAJI MZOEFU WA KIMATAIFA WA ZAMBIA, RODGERS KOLA KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top