• HABARI MPYA

  Saturday, July 31, 2021

  NYOTA WA R&B NCHINI, BEN POL ATOA NYIMBO NNE MPYA KALI TUPU AZIITA KIFURUSHI CHA B, ZAWADI KWA MASHABIKI WAKE

  NYOTA wa Muziki wa R&B nchini, Behnam Paul maarufu kama Ben Pol  amewazawadia mashabiki zake kifurushi chenye nyimbo Nne mpya (4)  alichokiita “B”.
  Ben Pol ameachia nyimbo hizo leo ambapo mojawapo amemshirikisha Msanii Billinas aliyoiita Kisebusebu, nyingine ni Unaita, For You na Warira ambayo tayari alishaiachia mapema mwezi huu.
  Msanii huyo amesema, ameamua kuita B kwa sababu inabeba stori na hali tofauti tofauti katika mapenzi kupitia nyimbo hizo nne.


  “Naamini jumbe zitaeleweka kwa watu wengi kwa kuwa ni mambo ambayo tunayaishi kila siku, 
  Upendo ndio jibu, na muziki ndio njia, nami namshukuru kila mmoja kwa Upendo na support yake kwangu” amesema Ben Pol
  Amesema kuwa bado anaendelea kuwashukuru mashabiki wake kwa kupokea nyimbo na kuendelea kufanya vizuri na amewaahidi kuendelea kuwapa ladha tofauti kila siku.
  B inapatikana katika mitandao yote ya muziki na vituo vya redio ndani na nje ya nchi.
  Nyimbo hizo zimetayarishwa katika studio za Pizzey Records na watayarishaji Chatta, O.righty na Jaco Beatz.        Mwisho
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NYOTA WA R&B NCHINI, BEN POL ATOA NYIMBO NNE MPYA KALI TUPU AZIITA KIFURUSHI CHA B, ZAWADI KWA MASHABIKI WAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top