• HABARI MPYA

  Tuesday, July 20, 2021

  POLISI TANZANIA YAACHANA NA WACHEZAJI WAKE 13 PAMOJA NA KUWAREJESHA KWENYE KLABU WOTE ILIYOKUWA INAWATUMIA KWA MKOPO

  TIMU ya Polisi Tanzania imetangaza kuachana na wachezaji wake 13 pamoja na kuwarejesha kwenye klabu zao nyota wote iliyokuwa inawatumia kwa mkopo baada ya msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ikimaliza nafasi ya sita.
  Afisa Habari na Mawasiliano wa Polisi Tanzania, Hassan Juma amewataja wachezaji hao kuwa ni Marcel Kaheza, Mohamed Bakari, Mohammed Yussuf, Mohammed Kassim, Ramadhani Kapele, Pato Ngonyani, Pius Buswita, Jimmy Shoji, Joseph Kimwaga, George Mpole, Emmanuel Manyanda, Erick Msagati na Hassan Nassor. 
  Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari, Polisi Tanzania imesema kuelekea msimu ujao itasajili wachezaji wapya wanane tu na kufanya jumla ya kikosi cha wachezaji 27, pamoja na 19 waliobaki sasa.


  Polisi Tanzania imemaliza nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kukusanya pointi 45 kwenye mechi 34 za msimu, nyuma ya KMC 48, Biashara United 50, Azam FC 68, Yanga SC 74 na mabingwa, Simba SC 83.   • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLISI TANZANIA YAACHANA NA WACHEZAJI WAKE 13 PAMOJA NA KUWAREJESHA KWENYE KLABU WOTE ILIYOKUWA INAWATUMIA KWA MKOPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top