• HABARI MPYA

    Monday, July 26, 2021

    MUKOKO TONOMBE AWAOMBA RADHI YANGA BAADA YA KUSABABISHA MAJANGA JANA KIGOMA TIMU IKICHAPWA 1-0 FAINALI ASFC

     KIUNGO wa Yanga SC, Mukoko Tonombe, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amewaomba radhi mashabiki wa timu yake pamoja na makocha baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
    Simba jana walifanikiwa kutetea taji la ASFC  baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya watani wa jadi, Yanga SC Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
    Yanga ililazimika kucheza pungufu tangu dakika ya 45 na ushei baada ya Muk
    oko kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumchezea rafu Nahodha wa Simba SC, John Raphael Bocco.
    Na baada ya hapo, kiungo wa kimafaifa wa Uganda, Thadeo Lwanga akafunga pekee la ushindi dakika ya 80 kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na kiungo wa kimafaifa wa Msumbiji, Jose Luis Miquissone.


    Ni taji la pili mfululizo la ASFC kwa Simba SC na taji la tatu la msimu, baada ya kubeba Ngao ya Jamii na ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mapema mwezi huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MUKOKO TONOMBE AWAOMBA RADHI YANGA BAADA YA KUSABABISHA MAJANGA JANA KIGOMA TIMU IKICHAPWA 1-0 FAINALI ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top