• HABARI MPYA

  Friday, July 30, 2021

  BODI YAAHIDI KUFANYIA MAREKEBISHO DOSARI ZILIZOJITOKEZA KATIKA MSIMU WA LIGI KUU YA TANZANIA BARA ULIOMALIZIKA ILI MSIMU UJAO MAMBO YAWE TOFAUTI


  BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeahidi kuzifanyia kazi changamoto zote zilizojitokeza katika msimu uliomalizika wa ligi hiyo ili msimu ujao mambo yawe mazuri.
  Katika taarifa yao ya shukrani baada ya msimu wa Ligi Kuu wa 2020-2021, Bodi imetoa shukrani kwa wadau mbalimbali, wakiwemo wadhamini waliofanya msimu huo ukamilike vyema.
  "Kwa umuhimu wa kipekee, Bodi imezichukua changamoto zote zilizojitokeza kwenye msimu wa 2020-2021 na kuahidi kuzifanyia kazi ili kuhakikisha msimu wa 2021-2022 unakuwa bora zaidi ya msimu huu tuliomaliza," imesema taarifa ya Bodi.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BODI YAAHIDI KUFANYIA MAREKEBISHO DOSARI ZILIZOJITOKEZA KATIKA MSIMU WA LIGI KUU YA TANZANIA BARA ULIOMALIZIKA ILI MSIMU UJAO MAMBO YAWE TOFAUTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top