• HABARI MPYA

  Tuesday, July 27, 2021

  NAOMI OSAKA ATUPWA NJE RAUNDI YA TATU TU TENISI OLMPIKI

  MJAPAN Naomi Osaka ametolewa katika Raundi ya Tatu tu kwenye Tenisi baada ya kuchapwa seti 2-0  (6-1, 6-4) na Marketa Vondrousova Jijini Tokyo mapema leo, hivyo kupoteza ndoto za kutwaa Medali ya Dhahabu nyumbani.
  China imeshinda Medali ya Dhahabu kwenye air pistol mixed mita 10 (kupiga pisto hewani kwa umbali wa mita 10), ikifuatiwa na Urusi iliyobeba Fedha, wakati Shaba imechukuliwa na Ukraine.
  Canada imeifunga Mexico 3-2 na kutwaa Medali ya Shaba katika kwenye softball, hiyo ikiwa medali yao ya kwanza kwenye mchezo huo.


  Owen Wright wa Australia ameshinda Medali ya kwanza ya Olimpiki kwenye Surfing (kucheza na kijimtumbwi) majini, akimbwaga Gabriel Medina kwa pointi 0.2 (11.97 to 11.77).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAOMI OSAKA ATUPWA NJE RAUNDI YA TATU TU TENISI OLMPIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top