• HABARI MPYA

  Saturday, July 24, 2021

  MTIBWA SUGAR NA COASTAL UNION ZAEPUKA JARIBIO LA KUSHUKA DARAJA BAADA YA KUZITUPA NJE PAMBA NA TRANSIT CAMP

  TIMU za Coastal Union na Mtibwa Sugar zimefanikiwa kusalia katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuzitoa Pamba na Transit Camp za Daraja la Kwanza katika mechi za mechi maalum za mchujo leo nyumbani.
  Coastal Union wameichapa Pamba FC mabao 3-1 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga na kubaki Ligi Kuu kwa ushindi wa jumla wa 5-3 baada ya sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza. 
  Sasa timu 16 zitakazoshiriki Ligi Kuu msimu ujao ni Simba SC, Yanga SC, Azam FC, Biashara United, KMC, Polisi Tanzania, Namungo, Tanzania Prisons, Dodoma Jiji FC, Ruvu Shooting, Mbeya City, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Coastal Union, Mbeya Kwanza na Geita Gold. 
  Mtibwa Sugar imelazimishwa sare ya 1-1 na Transit Camp Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na kusalia Ligi Kuu kwa ushindi wa jumla wa 4-2 kufuatia ushindi wa 4-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR NA COASTAL UNION ZAEPUKA JARIBIO LA KUSHUKA DARAJA BAADA YA KUZITUPA NJE PAMBA NA TRANSIT CAMP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top