• HABARI MPYA

  Saturday, July 10, 2021

  AZAM FC YAIONJESHA TRANSIT CAMP LADHA ZA LIGI KUU, YAICHAPA MABAO 2-1 LEO KATIKA MECHI YA KIRAFIKI CHAMAZI

  WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Transit Camp katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na viungo Frank Raymond Domayo dakika ya 40 na Valentino Mashaka Kusengama dakika ya 74 aliyepandishwa kutoka timu ya vijana, wakati la Trans Camp limefungwa na Khamis Salum dakika ya 77.
  Kwa Azam FC mchezo huu ni sehemu ya kujiweka sawa kwa mechi zake za mwisho za Ligi Kuu ya Tanzania Bara iliyofikia uingoni.


  Na Transit Camp inajiandaa kwa mchezo maalum wa mchujo wa kuwania kupanda Ligi Kuu dhidi ya moja ya timu mbili za ligi hiyo zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAIONJESHA TRANSIT CAMP LADHA ZA LIGI KUU, YAICHAPA MABAO 2-1 LEO KATIKA MECHI YA KIRAFIKI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top