• HABARI MPYA

  Sunday, July 18, 2021

  GIROUD ATUA MILAN BAADA YA MIAKA MITATU NA NUSU CHELSEA

  MSHAMBULIAJI Mfaransa, Olivier Jonathan Giroud amejiunga na AC Milan baada ya miaka mitatu na nusu ya kuwa na Chelsea.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 na mshindi wa Kombe la Dunia, anaondoka  Stamford Bridge alikotua Januari 2018 akitoka Arsenal ambako alidumu kwa miaka mitano na nusu.
  Alipokuwa na Chelsea, Giroud ameshinda mataji ya Kombe la FA, Europa League na Ligi ya Mabingwa katika mechi  119 alizocheza na kufunga mabao 39.
  Na wakati alipokuwa Arsenal alishinda mataji matatu ya FA  katika mechi 253 na kufunga mabao 105.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GIROUD ATUA MILAN BAADA YA MIAKA MITATU NA NUSU CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top