• HABARI MPYA

  Saturday, July 17, 2021

  UHONDO WA MECHI ZA KUHITIMISHA MSIMU WA LIGI KUU YA TANZANIA BARA KESHO NDANI YA AZAM TV, MECHO ZOTE LIVE

  MECHI tisa zinahitimisha msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara kesho na kuonyeshwa na chaneli mbalimbali za Azam Tv.
  Mechi kali zaidi itapigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kati ya JKT Tanzania yenye Danny Lyanga dhidi ya Mtibwa Sugar yenye Salum Kihimbwa. 
  JKT Tanzania wanalazimika kushinda ili angalau kuwania nafasi ya ‘play off’ huku wakiiombea mabaya Coastal Union, lakini Mtibwa Sugar nao wanahitaji angalau alama moja muhimu ili kujihakikishia nafasi ya ‘play-off’ huku nao wakiiombea mabaya Coastal Union. 
  Je, wewe utakuwa Mtibwa au JKT?
  Kwa kifurushi cha shilingi 20,000 unapata burudani hii mwezi mzima; Unachotakiwa kufanya ni kulipia mapema Kisimbuzi chako kuepuka usumbufu.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UHONDO WA MECHI ZA KUHITIMISHA MSIMU WA LIGI KUU YA TANZANIA BARA KESHO NDANI YA AZAM TV, MECHO ZOTE LIVE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top