• HABARI MPYA

  Sunday, July 04, 2021

  ARGENTINA YATINGA NUSU FAINALI COPA AMERICA, URUGUAY NJE

  TIMU ya taifa ya Argentina imetinga Nusu Fainali ya michuano ya Copa America kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ecuador Alfajiri ya leo Uwanja wa Pedro Ludovico Teixeira Jijini Goias, Brazil.
  Mabao ya Argentina yamefungwa Rodrigo De Paul dakika ya 40 na Lautaro Martínez dakika ya 84, wote wakimalizia pasi za Nahodha, Lionel Messi ambaye naye alishindilia msumari wa mwisho dakika ya 90 na ushei na sasa itakutana na Colombia iliyoitoa Uruguay kwa penalty 4-2 kufuatia sare ya 0-0 Uwanja wa Taifa wa Brasilia. 
  Nusu Fainali ya kwanza itakuwa Jumanne; Brazil na Peru, wakati Argentina na Colombia watamenyana na Jumatano. Brazil iliichapa Chile 1-0, bao pekee la Lucas Paqueta dakika ya 46 na Peru ilishinda kwa penalti 4-3 dhidi ya Paraguay kufuatia sare ya 3-3 usiku wa kuamkia jana.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARGENTINA YATINGA NUSU FAINALI COPA AMERICA, URUGUAY NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top