• HABARI MPYA

  Saturday, July 03, 2021

  BRAZIL YAICHAPA CHILE 1-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI COPA AMERICA

  WENYEJI, Brazil wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya michuano ya Copa America baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Chile, usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Nilton Santos Jijini Rio de Janeiro.
  Katika mchezo ambao wenyeji walimaliza wachache kufuatia Gabriel Jesus kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 48, bao pekee la Brazil limefungwa na Lucas Paqueta dakika ya 46. 
  Nayo Peru ilifanikiwa kwenda Nusu Fainali pia baada ya ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Paraguay  kufuatia sare ya 3-3 na itakutana na Brazil Jumanne.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BRAZIL YAICHAPA CHILE 1-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI COPA AMERICA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top