• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 23, 2021

  NGORONGORO HEROES YATUPWA NJE FAINALI ZA AFCON U20 BAADA YA KUCHAPWA 3-0 NA MOROCCO MAURITANIA

  TANZANIA imetupwa nje ya Fainali za Kombe la Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, AFCON U20 baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Morocco katika mchezo wa Kundi C jana Uwanja wa Olimpiki wa Nouakchott nchini Mauritania.
  Mabao ya Morocco yalifungwa na viungo El Mehdi Moubarik dakika ya nne kwa penalti, Mohammed Amine Essahel dakika ya nane na mshambuliaji Ayoub Mouloua dakika ya 13.
  Tanzania inamaliza na pointi moja nyuma ya Ghana iliyomaliza na pointi nne sawa na Gambia waliomaliza nafasi ya pili, wakati Morocco imeongoza kwa pointi zake saba.
  Ghana imefuzu Robo Fainali za AFCON U20 kama mshindi wa tatu bora zaidi ya washindi wa tatu wa makundi A na B.

  RATIBA YA ROBO FAINALI AFCON U20
  Alhamisi Februari 25, 2021
  Saa1:00 usiku
  Cameroon U20 Ghana U20
  Saa 4:00 usiku
  Burkina Faso U20 Uganda U20
  Ijumaa Februari 26, 2021
  Saa 1:00 usiku
  Morocco U20 Tunisia U20
  Saa 4:00 usiku
  Jamhuri ya Afrika ya Kati. U20 Gambia U20
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGORONGORO HEROES YATUPWA NJE FAINALI ZA AFCON U20 BAADA YA KUCHAPWA 3-0 NA MOROCCO MAURITANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top