• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 21, 2021

  CHELSEA YALAZIMISHA SARE YA 1-1 NA SOUTHAMPTON NGLAND


  KATIKA Ligi Kuu ya England, Chelsea jana imelazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, Southampton Uwanja wa St. Mary's, wenyeji wakitangulia kwa bao la Takumi Minamino dakika ya 33, kabla ya Mason Mount kuisawazishia The Blues kwa penalti dakika ya 54.
  Pamoja na sare hiyo, Chelsea inabaki nafasi ya nne kwa pointi zake 43 za mechi 25, nyuma ya Manchester United na Leicester City zenye pointi 46 za mechi 24 sawa na Manchester City inayoongoza kwa pointi 10 zaidi
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YALAZIMISHA SARE YA 1-1 NA SOUTHAMPTON NGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top