• HABARI MPYA

  Friday, February 12, 2021

  IHEFU SC YAWAZIMA RUVU SHOOTING PALE PALE MLANDIZI, YAWAPIGA 2-0 MCHANA KWEUPEE

  TIMU ya Ihefu SC ya Mbarali mkoani Mbeya leo imewaadhibu wenyeji,  Ruvu Shooting kwa kuwachapa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  Mabao ya Ihefu SC inayofundishwa na Zubery Katwila yamefungwa na Issa Ngoah yote dakika ya 21 na 90 na ushei na kwa ushindi huo inafikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi 19 na kusogea nafasi ya 16 katika ligi ya timu 20, ikiizidi pointi mbili tu Mbeya City inayoshika mkia kwa sasa.
  Ruvu Shooting iliyo chini ya kocha mzoefu, Charles Boniface Mkwasa inabaki na pointi zake 28 za mechi 19 sasa katika nafasi ya tano.
  Katika mechi iliyotangulia leo mchana, Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya KMC Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.


  Mabao ya Prisons yalifungwa na Jeremiah Juma Mgunda dakika ya 29 na 59, wakati la KMC limefungwa na Israel Patrick Mwenda dakika ya 37.
  Prisons inafikisha pointi 25 baada ya kucheza mechi 19 na kupanda nafasi ya saba, wakati KMC inabaki na pointi zake 25 za mechi 19 pia katika nafasi ya sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU SC YAWAZIMA RUVU SHOOTING PALE PALE MLANDIZI, YAWAPIGA 2-0 MCHANA KWEUPEE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top