• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 04, 2021

  MESSI KUWACHUKULIA HATUA WALIOVUJISHA MKATABA WAKE BARCA

  NYOTA wa Argentina, Lionel Messi anataka kulichukulia hatua za kisheria gazeti la El Mundo la Hispania kwa kuvujisha mkataba wake na FC Barcelona.  
  The El Mundo lilifanikiwa kuupata na kuuchapisha mkataba ambao Messi alisaini na klabu hiyo ya Katalunya mwaka 2017, ambao unaonyesha Messi analipwa dola Milioni 671 kwa zaidi ya miaka mine, kati ya hiyo dola Milioni 326 atalipa kodi.
  Messi anataka pia kuwachukulia hatua za kisheria washukiwa watano juu ya kuvuja kwa mkataba huo; Rais wa zamani wa Barca, Josep Maria Bartomeu; Makamu wa rais wa zamani, Jordi Mestre; Mtendaji Mkuu Oscar Grau; Kaimu Rais, Carles Tusquets na Mkuuwa Idara ya Sheria ya klabu, Roman Gomez Ponti.


  Mkataba huo wa Messi unamalizika Juni mwaka huu na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 atakuwa huru kuondoka. 
  Na jana Messi ameisaidia Barcelona kwenda Nusu Fainali ya Copa del Rey baada ya ushindi wa 5-3 dhidi ya Granada Uwanja wa Nuevo Los Carmenes, siku ambayo Levante nayo iliichapa Villarreal 1-0 na kusonga mbele.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI KUWACHUKULIA HATUA WALIOVUJISHA MKATABA WAKE BARCA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top