• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 12, 2021

  NGORONGORO HEROES WAENDA MAURITANIA KUCHEZA FAINALI ZA AFCON U20, WATAANZA NA GHANA JUMANNE


  TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imeondoka Dar es Salaam Alfajir ya leo kwenda Mauritania kwa ajili ya Fainali za AFCON U20 zinazoanza Jumapili hadi Machi 6.
  Ngorongoro imepangwa Kundi C pamoja na Ghana, Tanzania, Gambia na Morocco – na itafungua dimba na Ghana Jumanne kabla ya kucheza na Gambia Februari 19 na kumaliza na Morocco Februari 22, mecho zote Uwanja wa Manispaa ya Nouadhibou.
  juzi iliifunga Namungo FC 3-2 katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Azam Complex, Chamazi – mabao yake yakifungwa na Kelvin John mawili dakika ya sita na 26 na Abdul Khamis dakika ya 81, ya Namungo FC yakifungwa na Adam Salamba dakika ya 75 na 87.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGORONGORO HEROES WAENDA MAURITANIA KUCHEZA FAINALI ZA AFCON U20, WATAANZA NA GHANA JUMANNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top