• HABARI MPYA

  Monday, February 15, 2021

  NADAL ATINGA ROBO FAINALI MICHUANO YA AUSTRALIAN OPEN


  MSPANIOLA Rafael Nadal amekaribia rekodi ya taji la 21 la Grand Slam upande wa wanaume baada ya kumtoa mchezaji bora namba 16 duniani, Fabio Fognini seti 3-0 (6-3, 6-4, 6-2) na 
  kutinga Robo Fainali ya michuano ya Australian Open.
  Nadal sasa atakutana na ama mchezaji namba tano duniani, Stefanos Tsitsipas au namba tisa, Matteo Berrettini.
  Naye mchezaji bora namba 22 duniani, Jennifer Brady ametinga Robo Fainali yake ya kwanza ya michuano ya Australian Open baada ya kumfunga mchezaji namba 28, Donna Vekic wa Croatia seti 2-0 ( 6-1, 7-5) na sasa atakutana na Mmarekani mwenzake, Jessica Pegula.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NADAL ATINGA ROBO FAINALI MICHUANO YA AUSTRALIAN OPEN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top