• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 03, 2021

  MAN UNITED YAICHAPA SOUTHAMPTON 9-0 NA KUREJESHA MATUMAINI


  MANCHESTER United imeweka tena hai matumaini ya ubingwa baada ya ushindi wa mabao 9-0 jana dhidi ya Southampton iliyocheza pungufu ya wachezaji wawili kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford.
  Mabao ya Manchester United yamefungwa na Aaron Wan-Bissaka dakika ya 18, Marcus Rashford dakika ya 25, Jan Bednarek aliyejifunga dakika ya 34, Edinson Cavani dakika ya 39, Anthony Martial mawili dakika ya 69 na 90, Scott McTominay dakika ya 71, Bruno Fernandes dakika ya 87 kwa penalti na Dan James dakika ya 90 na ushei.
  Wachezaji wawili wa The Saints walitolewa kwa kadi nyekundu, Alexandre Jankewitz dakika ya pili na Bednarek dakika ya 86, kikosi cha Ralph Hasenhuttl kikichapwa 9-0 kwa mara ya pili ya msimu huu baada ya kupigwa pia Leicester
  United inarejea nafasi ya pili baada ya ushindi wa jana kwenye mechi ya 22, ikifikisha pointi 40, sawa na vinara, Manchester City wenye mechi mbili mkononi ambao wanaendelea kuongoza kwa wastani wao mzuri wa mabao
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAICHAPA SOUTHAMPTON 9-0 NA KUREJESHA MATUMAINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top