• HABARI MPYA

  Tuesday, February 16, 2021

  SERENA WILLIAMS ATINGA NUSU FAUNALI AUSTRALIAN OPEN


  MKONGWE Serena Williams ametinga Nusu Fainali ya Australian Open kwa ushindi wa seti mbili mfululizo (6-3, 6-3) dhidi ya mchezaji bora namba mbili duniani, Simona Halep leo Jijini Melbourne.
  Na katika kuwania taji la 24 la Grand Slam, mkongwe huyo mwenye umri wa 39 atamenyana na bingwa mtetezi, Naomi Osaka aliyemtoa Hsieh Su Wei seti mbili mfululizo (6-2, 6-2).
  Mchezaji namba 114, Mrusi Aslan Karatsev amekuwa mwanaume wa kwanza kutinga Nusu Fainali ya Grand Slam akimtoa namba 18, Grigor Dimitrov seti 3-1 (2-6, 6-4, 6-1, 6-2) na sasa atakutana na ama bingwa mtetezi, Novak Djokovic au Alexander Zverev 


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENA WILLIAMS ATINGA NUSU FAUNALI AUSTRALIAN OPEN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top