• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 15, 2021

  SIMBA SC YAREJEA DAR BAADA YA KUWAPIGA AS VITA KWAO MECHI YA UFUNGUZI MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

  KIKOSI cha Simba SC kimerejea jana Jijini Dar es Salaam kutoka Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambako Ijumaa walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, AS Vita katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Mabingwa hao wa Tanzania wanatarajiwa kuunganisha safari kwenda Musoma mkoani Mara kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Biashara United Alhamisi ijayo Uwanja wa Karume.
  Baada ya mechi hiyo watarudi Dar es Salaam kucheza mechi yake ya pili Kundi A Ligi ya Mabingwa dhidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly Februari 23 Uwanja wa Benjamin Mkapa.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAREJEA DAR BAADA YA KUWAPIGA AS VITA KWAO MECHI YA UFUNGUZI MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top