• HABARI MPYA

  Friday, February 12, 2021

  MRUNDI NDAYIRAGIJJE ATUPIWA VIRAGO TAIFA STARS BAADA YA TIMU KUTOLEWA MAPEMA CHAN

  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemfuta kazi kocha Mrundi wa timu ya taifa, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije wiki mbili baada ya Taifa Stars kutolewa mapema kwenye Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) nchini Cameroon.
  Taifa Stars ilimaliza nafasi ya tatu kwenye Kundi D nyuma ya Guinea na Zambia, matokeo ambayo hayakuiridhisha TFF na jana kutoa taarifa rasmi ya kuachana na Mrundi huyo.
  Ndayiragije aliteuliwa kuwa kocha wa Taifa Stars Julai mwaka 2019 akimpokea Mnigeria, Emmanuel Amunike na akaiwezesha Tanzania kurejea fainali za CHAN baada ya miaka 10 pamoja na kuivusha kwenye hatua ya makundi kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022 Qatar.
  Lakini mwenendo wa Taifa Stars si mzuri kwenye mbio za kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON, hadi sasa ikiwa inashika nafasi ya tatu kwenye Kundi J, nyuma ya Tunisia na Equatorial Guinea, mbele ya Libya.
  Hadi anaondolewa, Ndayiragijje kocha wa zamani wa Mbao FC ya Mwanza, KMC na Azam FC za Dar es Salaam ameiongoza Taifa Stars mechi 16, ikishinda tano, kati ya hizo  mbili kwa matuta, ikifungwa tano na sare sita.


  REKODI YA ETIENNE NDAYIRAGIJJE TAIFA STARS
  1. Tanzania 0-0 Kenya (Kufuzu CHAN- Dar es Salaam)
  2. Tanzania 0-0 (penalti 4-1) Kenya (Kufuzu CHAN – Nairobi)
  3. Tanzania 1-1 Burundi (Kufuzu Kombe la Dunia – Bujumbura)
  4. Tanzania 1-1 (Penalti 3-0) Burundi (Kufuzu Kombe la Dunia – Taifa)
  5. Tanzania 0-1 Sudan (Kufuzu CHAN – Taifa)
  6. Tanzania 0-0 Rwanda (Kirafiki Kigali)
  7. Tanzania 2-1 Sudan (Kufuzu CHAN – Omdurman)
  8. Tanzania 2-1 Equatorial Guinea (Kufuzu AFCON – Taifa)
  9. Tanzania 1-2 Libya (Kufuzu AFCON Tunisia)
  10. Tanzania 0-1 Burundi (Kirafiki Taifa)
  11. Tanzania 0-1 Tunisia (Kufuzu AFCON Tunisia)
  12. Tanzania 1-1 Tunisia (Kufuzu AFCON Benjamin Mkapa)
  13. Tanzania 1-1 DRC (Kirafiki Benjamin Mkapa)
  14. Tanzania 0-2 Zambia (CHAN 2021 – Limbe)
  15. Tanzania 1-0 Namibia (CHAN 2021 – Limbe)
  16. Tanzania 2-2 Guinea (CHAN 2021 – Douala)
  (Amekuwa kocha wa Taifa Stars kuanzia Julai 2019 hadi Februari 2021)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MRUNDI NDAYIRAGIJJE ATUPIWA VIRAGO TAIFA STARS BAADA YA TIMU KUTOLEWA MAPEMA CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top