• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 04, 2021

  MORRISON ATOA PASI YA BAO, AFUNGA LA USHINDI SIMBA SC YAWACHAPA DODOMA JIJI 2-1 JAMHURI

  MABINGWA watetezi, Simba SC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri Jijiji Dodoma.
  Kwa ushindi huo, Simba SC iliyocheza kwa mara ya kwanza katika ligi chini ya kocha mpya, Mfaransa Didier Gomes Da Rosa baada ya kuondokewa na Mbelgiji, Sven Ludwig Vandenbroeck inafikisha pointi 38 baada ya kucheza mechi 16 na kuendelea kushika nafasi ya pili nyuma ya watani wao wa jadi, Yanga SC wenye pointi 44 za mechi 18.


  Katika mchezo wa leo, winga Mghana Bernard Morrison alianza kumsetia mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere kufunga bao la kwanza dakika ya 30, kabla ya yeye mwenyewe kufunga la pili dakika ya 67 kwa pasi ya winga mpya, Perfect Chikwende aliyesajiliwa Januari kutoka FC Platinum ya kwao, Zimbabwe.
  Cleophase Mkandala akamalizia kazi nzuri ya Jamal Mtengeta dakika ya 36 kuipatia bao la kufutia machozi Dodoma Jiji FC.
  Dodoma Jiji FC inayofundishwa na kipa wa zamani wa Yanga SC, Mbwana Makatta inabaki na pointi zake 22 baada ya kucheza mechi 18 sasa ikiwa nafasi ya 10.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, KMC imeichapa Namungo FC 3-0, mabao ya Mathheo Anthony, Martin Ilamfya na Carlos Protas.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MORRISON ATOA PASI YA BAO, AFUNGA LA USHINDI SIMBA SC YAWACHAPA DODOMA JIJI 2-1 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top