• HABARI MPYA

  Sunday, February 07, 2021

  MANGUNGU MWENYEKITI MPYA WA SIMBA SC, AMGARAGAZA MBUNGE MWENZAKE WA ZAMANI, ALHAJ NKAMIA

  Na Asha Kigundula, DAR ES SALAAM
  MBUNGE wa zamani wa jimbo la Kilwa, Murtaza Ally Mangungu leo amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa klabu ya Simba baada ya kumshinda aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Alhaj Juma Nkamia, Mbunge wa zamani wa jimbo la Chemba, wote CCM katika uchaguzi uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
  Katika uchaguzi huo mdogo wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti, Swedi Nkwabi aliyejiuzulu Septemba 14, mwaka 2019, Mangungu alipata kura 802, sawa asilimia 70.3 dhidi ya mpinzani wake Nkamia aliyeipata kura 360, sawa na asilimia 28.9 katika zoezi lililohusiaha wanachama 1146, huku kura nane tu zikiharibika.
  Mapema katika mkutano huo, Mtendaji Mkuu wa klabu, Barbara Gonzalez alimtangaza Fatema Dewji kuwa mlezi wa timu ya wanawake, Simba Queens.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANGUNGU MWENYEKITI MPYA WA SIMBA SC, AMGARAGAZA MBUNGE MWENZAKE WA ZAMANI, ALHAJ NKAMIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top