• HABARI MPYA

  Saturday, February 06, 2021

  NGORONGORO HEROES YAFUTA UTEJA KWA UGANDA, YAICHAPA 5-3 KATIKA MECHI YA KIRAFIKI CHAMAZI


  TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imefuta uteja kwa Uganda baada ya ushindi wa 5-3 leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Tanzania inayofundishwa na kocha mzoefu, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ yamefungwa na Abdul Suleiman matatu dakika ya 14 na 89 kwa penalti na dakika ya 57, Kelvin John dakika ya 16 na Khamis Shaaban dakika ya 75, wakati ya Uganda yamefungwa na Ivan Kakoza dakika ya 20, Ivan Bogere dakika ya 26 na Samuel Ssenyonjo dakika ya 73.
  Mechi ya kwanza Uganda walishinda 1-0 Jumatano bao pekee la Ivan Bogere na michezo yote miwili ni maalum kwa timu hizo kujiandaa na Fainali za AFCON U20 zinazotarajiwa kufanyika nchini Mauritania kuanzia Februari 14 hadi Machi 4.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGORONGORO HEROES YAFUTA UTEJA KWA UGANDA, YAICHAPA 5-3 KATIKA MECHI YA KIRAFIKI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top