• HABARI MPYA

  Friday, February 26, 2021

  SIMBA SC YAENDELEA KUNG'ARA, YAWATANDIKA AFRICAN LYON 3-0 NA KUSONGA MBELE AZAM SPORTS FEDERATION CUP

  SIMBA SC imetinga Hatua ya 16 Bora michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya African Lyon leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na Ibrahim Ajibu mawili dakika ya 10 na 44 na Mzimbabwe Perfect Chikwende dakika ya 63, wakati Meddie Kagere alipiga nje penalti dakika ya 21 kuwakosesha Wekundu wa Msiimbazi bao lingine.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAENDELEA KUNG'ARA, YAWATANDIKA AFRICAN LYON 3-0 NA KUSONGA MBELE AZAM SPORTS FEDERATION CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top