• HABARI MPYA

  Thursday, February 18, 2021

  MAN CITY WAZIDI KUPAA ENGLAND BAADA YA KUIPIGA EVERTON 3-1


  TIMU ya Manchester City jana imeshinda 3-1 dhidi ya Everton FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Goodison Park.
  Mabao ya Man City yalifungwa na P. Foden dakika ya 32, R. Mahrez dakika ya 63 na Bernardo Silva dakika ya 77, wakati la Everton lilifungwa na Richarlison dakika ya 37.
  Kwa ushindi huo, Manchester City wamefikisha pointi 56 na sasa inaongoza Ligi Kuu kwa pointi 10 zaidi ya  Manchester United wanaofuatia baada ya timu zote kucheza mechi 24
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY WAZIDI KUPAA ENGLAND BAADA YA KUIPIGA EVERTON 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top