• HABARI MPYA

  Saturday, February 13, 2021

  SIMBA SC YAWADUWAZA AS VITA KWAO, YAWAPIGA 1-0 KINSHASA BAO PEKEE LA PENALTI LA MUGALU


  MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wameanza vyema hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, AS Vita Uwanja wa Martyrs de la Pentecote Jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo, Chriss Mugalu aliyeiadhibu timu ya nyumbani kwao kwa penalti dakika ya 61 baada ya beki wa AS Vita, Ousmane Adama Ouattara kuunawa mpira uliopigwa na kiungo Luis Miquissone, raia wa Msumbiji.
  Simba SC inatarajiwa kurejea Dar es Salaam kesho na kuunganisha safari Musoma mkoani Mara kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Biashara United Alhamisi ijayo Uwanja wa Karume.
  Itacheza mechi yake ya pili ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly Februari 23 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na katikati itakuwa na mechi nyingine ya ligi dhidi ya JKT Tanzania Machi 1 kabla ya kwenda kukamilisha mechi zake za mzunguko wa kwanza za ligi ya mabingwa kwa kucheza na wenyeji, Al Merreikh Machi 5 nchini Sudan.
  Kikosi cha AS Vita kilikuwa; O. Medjo, V. Assie Koua, O. Ouattara, D. Shabani, E. Sita, A. Masasi, P. Tshishimbi/ J. Mumbere dk57, S. Yacoub/ D. Moloko dk73, F. Mayele/Mayamba Mukokiani, F. Mayele dk57, J. Kalenda/ Z. Soze dk73 na M. Lilepo/R. Tulengi dk64.
  Simba SC; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Joash Onyango, Serge Wawa, Thadeo Lwanga, Larry Bwalya/Francis Kahata dk60 Clatous Chama/Kennedy Juma dk88, Luis Miquissone, Muzamil Yassin na Chirss Mugalu/ Meddie Kagere dk79.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAWADUWAZA AS VITA KWAO, YAWAPIGA 1-0 KINSHASA BAO PEKEE LA PENALTI LA MUGALU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top