• HABARI MPYA

  Wednesday, February 17, 2021

  CAF YAAMUA NAMUNGO NA PRIMIERO DE AGOSTO MECHI ZOTE MBILI ZICHEZWE TANZANIA NDANI YA SAA 72

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeamua mechi zote mbili za Kombe la Shirikisho kati ya Primiero de Agosto ya Angola  na Namungo FC ya Tanzania zichezwe nchini Tanzania.
  Uamuzi huo umefanywa baada ya Kamati ya CAF ya Mashindano hayo kubaini kuwa si Agosto wala Namungo iliyohusika moja kwa moja kukwamisha mechi ya kwanza iliyokuwa ichezwe Februari 14 nchini Angola.
  Mechi zote mbili zinatakiwa kuchezwa angalau ndani ya saa 72, na ziwe zimechezwa kufikia Februari 26 mwaka huu.

  Kwa mujibu wa ratiba, Primiero de Agosto ya Angola itakuwa mwenyeji wa mechi ya kwanza, hivyo itawajibika katika maandalizi yote ikiwemo gharama za maofisa wa mechi hiyo.
  Kwa vile makundi ya Kombe la Shirikisho yatapangwa Februari 22, mshindi wa jumla baada ya mechi hizo mbili hatazingatiwa katika viwango (non-ranked) wakati wa upangaji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF YAAMUA NAMUNGO NA PRIMIERO DE AGOSTO MECHI ZOTE MBILI ZICHEZWE TANZANIA NDANI YA SAA 72 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top