• HABARI MPYA

  Monday, February 08, 2021

  MANCHESTER CITY YAICHAPA LIVERPOOL 4-1 PALE PALE ANFIELD


  TIMU ya Manchester City jana wameichapa Liverpool 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield.
  Mabao ya Manchester City yalifungwa na Ilkay Gundogan mawili dakika ya 49 na 73, Raheem Sterling dakika ya 76 na Phil Foden dakika ya 83, wakati la Liverpool lilifungwa na Mohamed Salah kwa penalti  dakika ya 63.
  Kwa matokeo hayo, Manchester City inafikisha pointi 50 baada ya kucheza mechi 22 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya mahasimu wao, Manchester United ambao pia wamecheza mechi moja zaidi. 
  Mabingwa watetezi, Liverpool wanabaki nafasi ya nne wakiwa na pointi zao 40 za mechi 23, moja zaidi ya Chelsea na West Ham United baada ya wote kucheza mechi 23
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER CITY YAICHAPA LIVERPOOL 4-1 PALE PALE ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top