• HABARI MPYA

  Wednesday, February 24, 2021

  MSUVA ACHEZA KIPINDI KIMOJA WYDAD CASABLANCA YASHINDA 1-0 UGENINI LIGI YA MABINGWA

  KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana amecheza kipindi kimoja tu, timu yake Wydad Athletic Club, maarufu Wydad Casablanca ikiibuka na ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji, Petro Atletico Uwanja wa Novemba 11 Jijini Luanda nchini Angola.
  Msuva, mchezaji wa zamani wa Yanga ya nyumbani, Tanzania alimpisha Mohammed Ounajem mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya kuipigania Wydad kwa dakika 45.
  Na shujaa wa mchezo akawa Ayoub El Kaabi aliyefunga bao pekee kwenye mchezo huo wa Kundi C dakika ya 71 akimalizia pasi ya Muaid Ellafi.


  Ushindi huo unaifanya Wydad ipate pointi tatu za kwanza katika mchezo wake wa kwanza na sasa inashika nafasi ya pili nyuma ya Horoya ya Guinea yenye pointi za mechi mbili .
  Kaizer Chiefs iliyocheza mechi moja tu ikitoa sare ya 0-0 na Hoyora ina pointi moja, wakati Petro de Luanda inashika mkia baada ya kufungwa mechi zote mbili za kwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA ACHEZA KIPINDI KIMOJA WYDAD CASABLANCA YASHINDA 1-0 UGENINI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top