• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 04, 2021

  NGORONGORO HEROES YACHAPWA 1-0 NA UGANDA KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI CHAMAZI KUJIANDAA NA AFCON U20

  BAO pekee la Richard Bazangwa dakika ya 42 limeipa timu ya taifa ya Uganda ya vijana chini ya umri wa miaka 20, The Kobs ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania, Ngorongoro Heroes katika mchezo wa kirafiki usiku wa Jumatano Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Ulikuwa mchezo kati ya miwili baina ya tinu hizo kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (AFCON U20) baadaye mwezi huu nchini Mauritania.
  Timu hizo zitamenyana tena Jumamosi hapo hapo Chamazi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGORONGORO HEROES YACHAPWA 1-0 NA UGANDA KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI CHAMAZI KUJIANDAA NA AFCON U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top