• HABARI MPYA

  Sunday, February 14, 2021

  BORRUSIA DORTMUND YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA HOFFENHEIM


  KATIKA Bundesliga Borussia Dortmund jana imelazimishwa sare ya 2-2 na Hoffenheim, shukrani kwa Erling Haaland aliyeisawazishia dakika ya 81 Uwanja wa Signal-Iduna-Park, hilo likiwa bao la 16 la msimu kwa Mnorway huyo aliyefunga wakati mchezaji mmoja wa wapinzani akiwa ameanguka chini baada ya kuumia.
  Dortmund imeshinda mechi moja tu kati ya sita zilizopita za ligi na inajitoa tena kwenye Nne Bora katika mbio za kuwania tiketi ya Champions League na pengo linatarajiwa kuongezeka leo wakati Eintracht Frankfurt, Wolfsburg na Borussia Monchengladbach zikishuka dimbani.
  Kocha wa Dortmund, Edin Terzic tayari amekalia kuti kavu baada ya kufungwa mechi tatu kati ya nne za Bundesliga na amezidi kujiweka pagumu kufuatia kumuweka benchi Nahodha, Marco Reus
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BORRUSIA DORTMUND YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA HOFFENHEIM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top