• HABARI MPYA

  Thursday, February 25, 2021

  NAMUNGO FC YAKAMILISHA BIASHARA VIZURI NA KUTINGA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA BAADA YA KUWATOA WAANGOLA


  TIMU ya Namungo FC ya Ruangwa mkaoni Lindi imefanikiwa kwenda Hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika licha ya kufungwa 3-1 na Primiero do Agosto ya Angola jioni ya leo Uwanja ww Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Namungo FC inakwenda Hatua ya 16 Bora kwa ushindi wa jumla wa 7-5 baada ya kushinda 6-2 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam pia.
  Namungo inaingia Kundi D ambako itakuwa na Raja Casablanca ya Morocco, Pyramids FC ya Misri na Nkana FC ya Zambia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAKAMILISHA BIASHARA VIZURI NA KUTINGA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA BAADA YA KUWATOA WAANGOLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top