• HABARI MPYA

  Thursday, February 11, 2021

  BINGWA MTETEZI, SOFIA KENIN ATUPWA NJE AUSTRALIAN OPEN


  BINGWA mtetezi upande wa wanawake, Sofia Kenin ametupwa nje ya michuano ya Australian Open baada ya kufungwa seti mbili mfululizo (6-3, 6-2)ndani ya nusu saa kwenye mechi ya raundi ya Pili na Kaia Kanepi wa Estonia mapema leo Jijini Mebourne.
  Mkongwe wa Hispania, Feliciano Lopez akicheza mashindano yake ya 19 ya Australian Open amemtoa Mtaliano Lorenzo Sonego kwa seti 3-2 (5-7, 3-6, 6-3, 7-5, 6-4) katika mchezo uliodumu kwa saa tatu na dakika 18 sasa atamenyana na Andrey Rublev wa Urusi katika Raundi ya tatu 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BINGWA MTETEZI, SOFIA KENIN ATUPWA NJE AUSTRALIAN OPEN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top