• HABARI MPYA

  Sunday, February 07, 2021

  MTANZANIA AMCHAPA MGANDA PAMBANO LA KICKBOXING PTA

  MTANZANIA Emmnauel Shija jana amemshinda kwa pointi Ivan Kotela wa Uganda katika pambano la Kick Boxing kwenye usiku wa Vitasa Plus ukumbi wa PTA, Saba Saba Jijini Dar es Salaam.
  Naye Shaaban Katipwai akamdunda Bosco Ndiyeze Manzi wa Rwanda kwa Knickout (KO) ya raundi ya kwanza katika pambano la utangulizi. 
  Mapambano mengine ya utangulizi ya Kick Boxing yaliyowakutanisha Watanzania watupu, Ashraf Suleiman alimkong'ota Ally Ramadhan kwa KO ya raundi ya pili, Karim Kuchi akamdunda Said Matata kwa Technical Knockout (TKO) ya raundi ya tatu.


  Naye Chande Ally naye akamshinda Fundi Yusuph kwa TKO ya raundi ya kwanza, wakati Mrisho Rajab akafanikiwa kumshinda Sadam Ally kwa pointi.   
  Kulikuwa pia mapambano mawili ya Boxing na Ally Bakari akamtwanga Mohamed Muhunzi kwa pointi, wakati Shaaban Kaoneka alimchapa Kassim Pesa kwa TKO raundi ya nne.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTANZANIA AMCHAPA MGANDA PAMBANO LA KICKBOXING PTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top