• HABARI MPYA

  Friday, February 26, 2021

  KIM POULSEN AITA WACHEZAJI 43 KIKOSI CHA AWALI TAIFA STARS WAKIWEMO KELVIN YONDAN NA CHILUNDA  KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mdenmark Kim Paulsen ametaja kikosi cha awali cha wachezaji 43 kwa maandalizi ya mechi mbili za Kundi J kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Cameroon.
  Taifa Stars itasafiri kwenda Malabo kwa mchezo wa Machi 25 kabla ya kurejea nyumbani kuwakabili Equatorial Guinea Machi 28 katika mechi za kufuzu AFCON ya mwakani.
  Lakini kabla ya hapo kikosi hicho kitacheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya Kenya.
  Taifa Stars inahitahi kushinda mechi zote hizo ili kukata tiketi ya AFCON baada ya kuambulia ushindi mmoja na sare moja katika mechi zake nne za awali ilizocheza chini ya kocha Mrundi, Etienne Ndayiragijje aliyefukuzwa mapema mwezi huu.
  Kwa sasa Tanzania Taifa Stars inashika nafasi ya tatu Kundi J kwa pointi zake nne, moja zaidi ya Libya inayoshika mkia, wakati Tunisia yenye pointi 10 inaongoza ikifuatiwa na Equatorial Guinea yenye pointi sita.
  Wachezaji waliotwa kikosini ni makipa; Aishi Manula (Simba SC), Metacha Mnata (Yanga SC) na Juma Kaseja (KMC).
  Mabeki; Hassan Kessy (Mtibwa Sugar), Shomari Kapombe (Simba SC), Israel Mwenda (KMC), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC), Nickson KIbabage (Youssufia FC/Morocco), David Bryson (KMC), Yassin Mustapha (Yanga SC), Edward Manyama (Ruvu Shooting), Kennedy Juma (Simba SC), Erasto Nyoni (Simba SC), Dicksob Job (Yanga SC), Bakari Mwamnyeto (Yanga SC), Kelvin Yondan (Polisi Tanzania), Carlos Protas (Namungo FC) na Laurent Alfred (Azam FC).
  Viungo ni; Simon Msuva (Wydad Casablanca/Morocco), Hassan Dilunga (Simba SC), Muzamil Yassin (Simba SC), Jonas Mkude (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Feisal Salum (Yanga SC), Himid Mao (El Entag SC/Misri), Ally Msengi (Stellenbocsh FC/Afrika Kusini), Baraka Majogoro (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam FC), Farid Mussa (Yanga SC) na Iddi Suleiman ‘Nado’ (Azam FC).  
  Washambuliaji ni; Mbwana Samatta (Fenerebahce FC/Uturuki), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe/DRC), John Bocco (Simba SC), Yohanna Nkomola (Inhulets Petrove/Ukraine), Shaaban Iddi Chilunda (Moghreb FC/Morocco), Ditram Nchimbi (Yanga SC), Deus Kaseke (Yanga SC)Abdul Suleiman (Coastal Union), Kelvin John (Brook House College/England), Nassor Saadun Hamoud (MFK/Czech) na Meshack Abraham (Gwambina FC).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIM POULSEN AITA WACHEZAJI 43 KIKOSI CHA AWALI TAIFA STARS WAKIWEMO KELVIN YONDAN NA CHILUNDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top