• HABARI MPYA

  Friday, February 12, 2021

  BAYERN WATWAA KLABU BINGWA YA DUNIA, NI TAJI LA SITA LA MSIMU


  MABINGWA wa Ulaya, Bayern Munich wamefanikiwa kutwaa taji la Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa wa Amerika Kaskazini, Tigres UANL ya Mexico usikiu wa jana Uwanja wa Education City Jijini Al Rayyan, Qatar. 
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Benjamin Pavard dakika ya 59 akimalizia mpira uliookolewa na kipa wa Tigres, Nahuel Guzman kufuatia kichwa cha Robert Lewandowski.
  Hilo linakuwa taji la sita la msimu kwa Bayern Munich baada ya awali kubeba ubingwa wa Ligi, yaani Bundesliga, makombe yote mawili ya Ujerumani, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Super Cup
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAYERN WATWAA KLABU BINGWA YA DUNIA, NI TAJI LA SITA LA MSIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top