• HABARI MPYA

  Thursday, February 18, 2021

  MORRISON AING'ARISHA SIMBA SC MUSOMA, AFUNGA BAO PEKEE LA USHINDI DHIDI YA BIASHARA UNITED

  Na Asha Said, MUSOMA
  BAO pekee la winga Mghana, Benard Morrison dakika ya 22 leo limetosha kuipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Biashara United Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
  Morrison alifunga bao hilo baada ya shambulizi kali kupitia kwa winga Mzimbabwe, Perfect Chikwende, aliyesaidiana na beki na beki Mkenya, Joash Onyango na kiungo mzawa, Said Ndemla.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 18, sasa wakizidiwa pointi nne na vinara, Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi mbili zaidi.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, JKT Tanzania imelazimishwa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


  JKT walitangulia kwa bao la Daniel Lyanga dakika ya 45, kabla ya Marcel Kaheza kuisawazishia Polisi dakika ya 69, mabao yote yakipatikana kwa mikwaju ya penalti.
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo unafuatia baadaye Saa 1:00 usiku kati ya Azam FC na Mbeya City Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Kikosi cha Biashara United kilikuwa; James Ssetuba, Denis Nkame, Mpapi Nassib,  Lenny Vedastus, Abdulmajid Mangaro, Baraka Makoba,  Ibrahim Isihaka,  Ramadhan Chombo,  Deogratius Judika, Christian Zzigah/Gerson Kabeja dk63 na Tariq Simba. 
  Simba SC; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gaediel Michael/Mohammed Hussein 'Tshabalala' dk57, Joash Onyango,  Pascal Wawa, Thadeo Lwanga,  Parfect Chikwende, Muzamil Yassin, Said Ndemla/Clatous Chama dk68,  Medie Kagere na Benard Morrison/Hassan Dilunga dk79.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MORRISON AING'ARISHA SIMBA SC MUSOMA, AFUNGA BAO PEKEE LA USHINDI DHIDI YA BIASHARA UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top