• HABARI MPYA

  Friday, February 12, 2021

  CHELSEA YATINGA ROBO FAINALI FA, KUUMANA NA SHEFFIELD UNITED


  BAO pekee la Tammy Abraham dakika ya 64, jana liliipa Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Barnsley katika mchezo wa Raundi ya Tano Kombe la FA England Uwanja wa Oakwell, Barnsley, South Yorkshire.
  Chelsea inatinga Robo Fainali na sasa itakutana na Sheffield United Uwanja wa Stamford Brodge, London wakati Robo Fainali nyingine Everton itakuwa mwenyeji wa Manchester City, Leicester wataikaribisha Manchester United na Bournemouth watakuwa wenyeji wa Southampton.
  Mechi hizo zitachezwa wikiendi ya Machi 20 na 21 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YATINGA ROBO FAINALI FA, KUUMANA NA SHEFFIELD UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top