• HABARI MPYA

  Friday, February 19, 2021

  NGORONGORO HEROES YAOKOTA POINTI YA KWANZA AFCON U20 BAADA YA SARE YA 1-1 NA GAMBIA LEO NCHINI MAURITANIA


  TANZANIA imeokota pointi ya kwanza katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (AFCON U20) baada ya sare ya 1-1 na Gambia katika mchezo wa Kundi C leo Uwanja wa Manispaa ya Nouadhibou nchini Mauritania.
  Gambia walitangulia kwa bao la Momodou Bojang dakika ya 40, kabla ya Novatus Dismas kuisawazishia Ngorongoro Heroes dakika ya 87.
  Mechi nyingine ya kundi hilo, Morocco ililazimishwa sare ya 0-0 na Ghana hapo hapo Uwanja wa Manispaa ya Nouadhibou.
  Ghana inaendelea kuongoza Kundi C kwa ponti zake nne sawa na Morocco ikiwa kileleni kwa wastani wa mabao, wakifuatiwa na Gambia yenye pointi moja sawa na Tanzania. 
  Tanzania iliyochapwa 4-0 na Ghana katika mechi yake ya kwanza, itakamilisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na Morocco Jumanne ijayo kuangalia mustakabali wake wa kusonga mbele.
  Gambia iliyochapwa 1-0 na Morocco katika mchezo wa kwanza itamaliza na Ghana. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGORONGORO HEROES YAOKOTA POINTI YA KWANZA AFCON U20 BAADA YA SARE YA 1-1 NA GAMBIA LEO NCHINI MAURITANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top