• HABARI MPYA

  Monday, February 15, 2021

  AUBAMEYANG APIGA HAT TRICK ARSENAL YAICHAPA LEEDS 4-2


  TIMU ya Arsenal jana imeifunga Leeds United 4-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates, London.
  Nahodha Pierre-Emerick Aubameyang alifunga matatu dakika ya 13 akimalizia pasi ya Granit Xhaka, dakika ya 41 kwa penalti na 47 akimalizia pasi ya Emile Smith Rowe, wakati lingine limefungwa na Hector Bellerin dakika ya 45 na ya Leeds yamefungwa na Pascal Struijk dakika ya 58 na Helder Costa dakika ya 69.
  Arsenal inafikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 24 na kusogea nafasi ya 10, wakati Leeds inayobaki na pointi zake 32 za mechi 23, inashukia nafasi ya 11 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AUBAMEYANG APIGA HAT TRICK ARSENAL YAICHAPA LEEDS 4-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top