• HABARI MPYA

  Monday, February 22, 2021

  NAMUNGO FC YATANGULIZA MGUU MMOJA HATUA YA MAKUNDI YA KOMBE LA SHIRIKISHO BAADA YA KUICHAPA 1 PRIMIERO DE AGOSTO 6-2

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Namungo FC imetanguliza mguu mmoja hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 6-2 dhidi ya Primiero de Agosto ya Angola katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua hiyo ya 16 Bora ya michuano hiyo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Mabao ya Namungo yalifungwa na Hashim Manyanya dakika ya 32, Sixtus Sabilo dakika ya 38 na 59, Reliants Lusajo dakika ya 55, Erick Kwizera dakika ya 66 na Stephen Sey dakika ya 72.
  Mechi ya marudiano itapigwa ndani ya saa 72 zijazo Tanzania pia, na Namungo itahitaji sare au kufungwa si zaidi ya mabao 4-0 ili kuingia hatua ya makundi ya michuano hii ya Kombe la Shirikisho,
  Hiyo ni baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuamua mechi zote mbili za mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho kati ya CD 1 Agosto ya Angola na Namungo FC zichezwe nchini Tanzania.


  Maamuzi hayo yalifuatia Kamati ya Mashindano CAF ya kubaini kuwa si Agosto wala Namungo iliyohusika moja kwa moja kukwamisha mechi ya kwanza iliyopangwa ichezwe Februari 14 nchini Angola na kupanga mechi zote mbili zichezwe angalau ndani ya saa 72 kufikia Februari 26 mwaka huu huku CD 1 Agosto ikipangwa kuwa mwenyeji kwenye mechi ya kwanza.
  Tatizo lilianzia Serikali ya Angola kutaka kuwaweka karantini wachezaji wote wa Namungo FC kabla ya mchezo wa kwanza Februari 14 uliopangwa kufanyika Uwanja wa Novemba 11 Jijini Luanda, ikidai watatu kati yao wamekutwa na virusi ya corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID 19.
  Hao ni Hao ni Lucas Kikoti, Fred Tangalu na Khamis Faki pamoja na Mtendaji Mkuu, Omar Kaaya. Namungo ikifuzu itakuwa mara ya kwanza kwa Tanzania kuingiza timu zote mbili hatua ya makundi ya michuano ya Afrika msimu mmoja, kwani tayari Simba SC ipo Kundi A kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YATANGULIZA MGUU MMOJA HATUA YA MAKUNDI YA KOMBE LA SHIRIKISHO BAADA YA KUICHAPA 1 PRIMIERO DE AGOSTO 6-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top