• HABARI MPYA

    Tuesday, February 23, 2021

    SIMBA SC YAITWANGA AL AHLY YA MISRI 1-0 NA KUPANDA KILELENI KUNDI A LIGI YA MABINGWA AFRIKA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MABINGWA wa Tanzania, Simba Sports Club wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. 
    Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee dakika ya 31, kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone kwa shuti la umbali wa mita 20 baada ya kuwahadaa viungo wa Ahly  Aliou Dieng, raia wa Mali na Mmisri Akram Tawfik kufuatia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chota Chama.
    Kwa ushindi huo, Simba inayofundishwa na kocha Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa inafikisha pointi sita baada ya kucheza mechi mbili kufuatia ushindi wa ugenini wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya AS Vita mjini Kinshasa Febaruari 12.


    Baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, E l Merreikh leo Uwanja wa Al-Hilal Jijini Omdurman, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inakaa nafasi ya pili ikilingana pointi na Al Ahly.
    Mechi ijayo SImba SC watakuwa wageni wa El Merreikh nchini Sudan na Al Ahly watakuwa wenyeji wa AS Vita Jijini Cairo Machi 5, mwaka huu.
    Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Joash Onyango, Pascal Wawa, Thadeo Lwanga/Erasto Nyoni dk71, Luis Miquissone/Francis Kahata dk88, Muzamil Yassin, Chriss Mugalu/Meddie Kagere dk87, Clatous Chama na Hassan Dilunga/Larry Bwalya dk46.
    Al Ahly; Mohamed El Shenawy, Mahmoud Waheed/ Ayman Ashraf dk85, Yasser Ibrahim, Mohamed Hany, Badr Banoun, Aliou Dieng, Hamdi Fathi, Akram Tawfik/ Mohamed Sherif dk78, Mahmoud Soliman ‘Kahraba’/ Mohamed Magdi Kafsha dk60, Oluwafemi Ajayi/ Marwan Mohsen dk78 na Walter Bwalya/Amr Al Sulaya dk60.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAITWANGA AL AHLY YA MISRI 1-0 NA KUPANDA KILELENI KUNDI A LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top