• HABARI MPYA

  Thursday, February 11, 2021

  NGORONGORO HEROES YAWACHAPA NAMUNGO FC 3-2 KATIKA MECHI YA KIRAFIKI LEO CHAMAZI

  TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes Jumatano jioni imeifunga Namungo FC 3-2 katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. 
  Mabao ya Ngorongoro Heroes yamefungwa na Kelvin John mawili dakika ya sita na 26 na Abdul Khamis dakika ya 81, wakati ya Namungo FC yamefungwa na Adam Salamba yote mawili dakika ya 75 na 87.
  Namungo imeutumia mchezo huo kama maandalizi ya mwisho kabla ya kwenda kumenyana na wenyeji, Primiero de Agosto ya Angola Jumapili Jijini Luanda katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.


  Kwa Ngorongoro Heroes mchezo huo ulikuwa maandalizi ya mwisho kabla ya Alhamisi kusafiri kwenda Mauritania kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, AFCON U20. michuano inayotarajiwa kuanza Jumapili hadi Machi 4.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGORONGORO HEROES YAWACHAPA NAMUNGO FC 3-2 KATIKA MECHI YA KIRAFIKI LEO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top