• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 01, 2021

  KOEMAN ATAKA ALIYEVUJISHA MKATABA WA MESSI AFUKUZWE

  KOCHA wa Barcelona, Ronald Koeman ameagiza uchunguzi ufanyike juu ya kuvuja kwa mkataba kwa Lionel Messi na aliyefanya hivyo kama anatika ndani ya uongozi wa klabu aondolewe.
  Gazeti la El Mundo jana limeripoti kwamba Lionel Messi amelipwa zaidi ya dola za Kimarekani Milioni 673, katika mkataba wake wa sasa wa miaka minne Barcelona aliosaini mwaka 2017 ambayo ni sawa na dola Milioni 167 kwa mwaka – huo ukiwa mkataba mnono zaidi kihistoria kwa wanamichezo.
  Messi amekuwa mchezaji wa Barcelona kwa karibu miongo miwili sasa, lakini aliomba kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita akisema hafurahishwi na mwelekeo wa klabu kwa sasa, ingawa ombi lake lilikataliwa – atakuwa huru kuondoka mwishoni mwa msimu huu.


  Messi jana amefunga bao la kwanza dakika ya 20, Barcelona ikiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Athletic Bilbao Uwanja wa Camp Nou, bao la pili likifungwa na  Antoine Griezmann dakika ya 74, wakati la Bilbao lilifungwa na  Jordi Alba aliyejifunga dakika ya  49.
  Barcelona imefikisha pointi 40 sawa na Real Madrid na wanapanda nafasi ya pili kwa wastani mzuri wa mabao baada ya timu zote kucheza mechi 20 na wote wapo nyuma na Atletico Madrid yenye pointi 50 za mechi 19 tu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOEMAN ATAKA ALIYEVUJISHA MKATABA WA MESSI AFUKUZWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top